Machapisho

Machapisho yenye alama ya ♦ husomekana moja kwa moja, kwenye muundo wa mwisho. Kwa machapisho mengine, ukishindwa kuyapata, wasiliana nami, na nitakutuma nakala.

♦ Andrason, Alexander, and Andrew Harvey. 2024. Instability of interactives: The case of interjections in Gorwaa. In: Open Linguistics, 10(1), 20240033. DOI: <10.1515/opli-2024-0033>

Muhtasari
Makala haya huchunguza ukosefu wa uthabiti wa mofo-fonetiki ya viingiliano (yaani: interactives) kupitia mfano wa vihisishi (yaani: interjections) vya Kigorowa. Uchanganuzi wa miundo 91 unaonyesha kwamba, katika Kigorowa, vihisishi ni visivyo thabiti sana: idadi ya vihisishi vya mitindopeke (yaani: idiolectal) ni kubwa zaidi kuliko ile ya vihisishi vinavyoshirikwa kati ya wazungumzaji, na vihisishi vya seti zote mbili huunda nguzo – nafasi zinazoundwa na miundo iliyounganishwa kupitia kufanana kwa familia. aina rasmi na ya kazi. Marekebisho rasmi yanaafikiwa kupitia kurefusha, urudufishaji, ubadilishaji (wa simu/vipengele), na upatanisho, na yanahusiana na mabadiliko ya maana na polisemia asilia kwa vihisishi. Kwa jumla, kundi la kihisishi limeundwa kama mtandao unaobadilikabadilika wa miundo inayohusiana (kiumbo/kitendo). Wasifu wa kisarufi wa vihisishi vilivyoshirikiwa na vya mitindopeke vinafanana na vinathibitisha uhalali wa mfano wa vihisishi. Maboresho yaliyopendekezwa ni pamoja na upendeleo wa [j] zaidi ya [w], mwelekeo wa toni za juu sana, na mifumo ya toni inayopungua, matumizi ya sauti zinazotenlenezwa kwenye koo kama sauti za kawaida na vidoko (yani: clicks) kama konsonanti halisi katika lugha zisizo za vidoko, msingi wa tanakali (yaani: iconic) wa baadhi ya vihisishi na uhusiano wao na lugha ya watoto (yaani: babytalk), pamoja na uhusiano wa karibu wa vihisishi na mahali pa kutamka pa |A|.

Andrason, Alexander, Andrew Harvey & Richard Griscom. (2023). The form of emotions: the phonetics and morphology of interjections in Hadza. In: Poznan Studies in Contemporary Linguistics. DOI: 10.1515/psicl-2022-1037

Muhtasari
Chapisho hiki hutoa uchambuzi wa kwanza kuhusu umbo (kifonetiki na kimofolojia) wa vihisishi vya Kihadzabe. Kwa kutumia methodolojia ya umbo kamili (yaani: prototype approach) kwa aina ya kihisishi na kwa kutumia data mpya, waandishi huonyesha kwamba vihisishi vya Kihadzabe hufuata umbo kamili wa kihisishi karibu sana. Vihisishi vya Kihadzabe vina sifa za umbo kamili na vinavyokuwa tofauti, tofauti hizi hufanana na tofauti zilizotambuliwa kwenye lugha tofauti. Kwa kiasi kubwa, utafiti huu huimarisha wazo la umbo kamili uliyotolewa kwenye utafiti wengine, lakini maelezi zaidi kadhaa hutolewa.

♦ Sands, Bonny, Andrew Harvey, Maarten Mous, and Mauro Tosco. 2023. Why Hadza is (probably) not Afroasiatic: a discussion of Militarev’s “Hadza as Afrasian?” Journal of Language Relationship • Вопросы языкового родства • 21:1–2. pp. 91–109. Link: https://jolr.ru/files/(334)jlr2023-21-1-2(91-109).pdf

Muhtasari
Hapo tunatazama tatizo na ushuhuda wa kileksika uliyotumia kudai kwamba lugha ya Kihadzabe ni kwenye familia ya Afroasiatiki. Kushindwa kuyatambua maneno kopo na shida kwenye uchambuzi wa mofimu za Kihadzabe ni tatizo zinazoondolewa kwa kuwa na ufahamu ukubwa zaidi na Kihadzabe na historia yake ya mgusano. Tatizo zingine zinazohusika na methodolojia iliyotumika. Viwanja vya kisemantiki vinavyoruhusiwa kutambulisha vikundi vya umbile-maana huongeza hatari ya maneno kufanana kwa bahati tu. Utumiaji wa maneno yanayoweza kuwa onomatopia yanafifisha vikundi umbile-maana pia. Mwishoni, ni ukosefu wa sauti zinazoendana kati ya Kihadzabe na lugha za Afroasiatiki unayofanya pendekezo huu la kuweka Kihadzabe kwenye familia ya Afroasiatiki kushindwa kushawishi.

♦ Harvey, Andrew, Gibson, Hannah and Griscom, Richard. “Preverbal clitic clusters in the Tanzanian Rift Valley revisited” Journal of African Languages and Linguistics, vol. 44, no. 2, 2023, pp. 175-239. DOI: 10.1515/jall-2023-2010

Muhtasari
Chapisho hiki huangalia vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi kwenye Bonde la Ufa la Tanzania, eneo lenye anuwai ya lugha kubwa sana, na lugha kutoka familia za Kibantu, Kikushi, Kiniloti, pamoja na Kisandawe (kinachoweza kuwa na mnasaba na lugha za familia ya Khoi-Kwadi), na lugha kisiwa ya Kihadzabe. Kazi mmoja ya mapema zaidi (Kießling, Roland, Maarten Mous & Derek Nurse. 2007. The Tanzanian Rift Valley area. In Bernd Heine & Derek Nurse (eds.), A linguistic geography of Africa, 186–227. Cambridge: Cambridge University Press) ilivitambua vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi kama sifa bainifu kwenye lugha nyingi za “Eneo la Bonde la Ufa la Tanzania”. Chapisho hiki hutoa taarifa zaidi kuhusu vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi kwenye lugha za eneo hili, pamoja na kuchunguza njia za ukuzaji wa viunzi hivi. Kutokana na uchambuzi huu, picha inayopatikana ni yenye changamani: mipangilio ya matukio hayawezi kuweka Kikushi cha Ufa Magharibi (yaani: West Rift Cushitic) au lugha zake tangulizi kama mtindo kwa ukuzaji pekee wa vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi, na, kwa Kisandawe (na labda lugha za Kidatooga), inaonekana kwamba ukuzaji wa vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi hauwezi hata kuelezwa kama tokeo ya mgusano wa lugha. Kuhusu uwezo wa Bonde la Ufa la Tanzania kuwa “kundi eneo”, chapisho hiki huacha mazungumzo wa jiografia na hoja kwa au dhidi ya “Kundi Eneo la Bonde la Ufa la Tanzania” na huongea zaidi kuhusu matukio moja moja ya kihistoria (linganisha Campbell, Lyle. 2017. Why is it so hard to define a linguistic area? In Raymond Hickey (ed.), The Cambridge handbook of areal linguistics, 19–39. Cambridge: Cambridge University Press) yaliyoweza kusaidia ukuzaji wa vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi kwenye lugha sampuli yetu, na vile vile hutumainisha uchunguzi zaidi kwenye historia hizi kwa vifaa vya isimu lakini vile vile za masomo mbalimbali.

♦ Sands, Bonny; Harvey, Andrew; and Griscom, Richard (2023) “Reconnecting through language in Africa,” Living Languages • Lenguas Vivas • Línguas Vivas: Vol. 2: No. 1, Article 6. DOI: 10.7275/vktz-cy05

Muhtasari
Chapisho hili huangalia kazi za jamii mbalimbali kukaribiana kwa njia ya lugha barani Afrika. Mkaguzi huu hupangwa kwa eneo la kijiografia (Afrika Kaskazini-Mashariki, Afrika Mashariki, Afrika Kusini, na Afrika Magharibi) na pia lina sehemu ndogo inayotazama kazi ya kufufua mifumo ya kuandika ya Kiafrika. Mifano tunayoangalia ni: Kikoptiki (yaani: Coptic), Kige‘ez, Kiyaaku, Kielmolo, Kima’a (yaani: Kimbugu cha Ndani), Kicape Khoekhoe, Kinǀuu, Kitjwao, na Chingoni. Mifano ya mifumo ya kuandiki tunayoangalia ni: Kitifinagh, na Kinubi.

♦ Didier Demolin, Alain Ghio, Andrew Harvey. Acoustic and Aerodynamic Features of Hadza Clicks. In: 20th International Congress of Phonetic Sciences, 2023, Prague, Czech Republic. pp. 3387-3391. Kiungo: https://hal.science/hal-04248345     Pakua

Muhtasari
Lugha ya Kihadzabe ina sauti za vidoko 4 miongoni wa sauti zake: kidoko cha midomo, kidoko cha meno, kidoko cha ufizi, na kidoko cha bapa la ulimi [ʘ, |, !, ‖] vinavyoweza kutengenezwa na mpumuo, na glota, na nazali [ʘ̰, |ʔ, |h, ɴ|, ɴ|ʔ, !ʔ, !h, ɴ!, ɴ!ʔ, ‖, ‖h, ɴ‖h, ɴ‖ʔ]. Kidoko cha midomo [ʘ] huachwa wazi na kelele na huelezwa kama [grave & noisy]. Kiakoustika, vidoko vya kinywa [|, !, ‖] huelezwa na sifa mbili [grave au acute] na [abrupt au noisy]. Sifa ya [grave] hubaini kidoko cha ufizi [!] ina kilele kwenye kipimo cha FFT karibu ya 2 kHz. Sifa ya [acute] hubaini vidoko vya meno na bapa la ulimi [|, ‖] ina kilele karibu ya 6 kHz kwa kidoko cha meno na kwa kidoko cha bapa la ulimi kilele kati ya 4 na 5 kHz. Vile vile, tofauti kati ya [abrupt] [!, ‖] ina sifa ya urefu: pasuo fupi au pasuo sauti kanda.

♦ Hedvig Skirgård et al. 2023. Grambank reveals the importance of genealogical constraints on linguistic diversity and highlights the impact of language loss. Science Advances 9. DOI:10.1126/sciadv.adg6175    Pakua

Waandishi Wote
Hedvig Skirgård, Hannah J. Haynie, Damián E. Blasi1, Harald Hammarström, Jeremy Collins, Jay J. Latarche, Jakob Lesage, Tobias Weber, Alena Witzlack-Makarevich, Sam Passmore, Angela Chira, Luke Maurits, Russell Dinnage, Michael Dunn, Ger Reesink, Ruth Singer, Claire Bowern, Patience Epps, Jane Hill, Outi Vesakoski, Martine Robbeets, Noor Karolin Abbas, Daniel Auer, Nancy A. Bakker, Giulia Barbos, Robert D. Borges, Swintha Danielsen,Luise Dorenbusch, Ella Dorn, John Elliott, Giada Falcone, Jana Fischer,Yustinus Ghanggo Ate, Hannah Gibson, Hans-Philipp Göbel, Jemima A. Goodall, Victoria Gruner, Andrew Harvey, Rebekah Hayes, Leonard Heer, Roberto E. Herrera Miranda, Nataliia Hübler, Biu Huntington-Rainey, Jessica K. Ivani, Marilen Johns, Erika Just, Eri Kashima, Carolina Kipf, Janina V. Klingenberg, Nikita König, Aikaterina Koti, Richard G. A. Kowalik, Olga Krasnoukhova, Nora L. M. Lindvall, Mandy Lorenzen, Hannah Lutzenberger, Tânia R. A. Martins, Celia Mata German, Suzannevan der Meer, Jaime Montoya Samamé, Michael Müller, Saliha Muradoglu, Kelsey Neely, Johanna Nickel, Miina Norvik, Cheryl Akinyi Oluoch, Jesse Peacock, India O.C. Pearey, Naomi Peck, Stephanie Petit, Sören Pieper, Mariana Poblete, Daniel Prestipino, Linda Raabe, Amna Raja, Janis Reimringer, Sydney C. Rey, Julia Rizaew, Eloisa Ruppert, Kim K. Salmon, Jill Sammet, Rhiannon Schembri, Lars Schlabbach, Frederick W. P. Schmidt, Amalia Skilton, Wikaliler Daniel Smith, Hilário de Sousa, Kristin Sverredal, Daniel Valle, Javier Vera,  Judith Voß, Tim Witte, Henry Wu, Stephanie Yam, Jingting Ye, Maisie Yong, Tessa Yuditha, Roberto Zariquiey, Robert Forkel, Nicholas Evans, Stephen C. Levinson, Martin Haspelmath, Simon J. Greenhill, Quentin D. Atkinson, Russell D. Gray
Muhtasari
Wakati mapangilio ya anuwai ya kijenetiki ya wanadamu yanaendelea kuelewa kwa ndani, anuwai ya lugha bado haielezwi kivile. Hapo ndani, tunaeleza mkusanyiko wa data wa Grambank. Grambank ina mifano 400,000 za data kwa lugha 2,400 na ni mkusanyiko mkubwa wa data za kulinganisha kuliko yote yanayopatikana. Ukubwa wa Grambank hutuwezesha kupima athari za uridhi wa kijenetiki na umbali wa kijiografia kwa anuwai ya umbile wa lugha za dunia, kuangalia vizuizi vya anuwai kiisimu, na kutambua lugha tofauti sana duniani. Uchambuzi wa matokeo ya kupoteza lugha huonyesha kwamba upungufu wa anuai haitakuwa sawa kwenye mikoa ya lugha duniani. Bila kazi kubwa kurekodi na kufufua lugha zinazohatarishwa, dirisha letu la kiisimu kwenye historia, fikra, na utamaduni za binadamu utavunjwa vibaya.

Harvey, A. (2020). H. Ekkehard Wolff (ed.): The Cambridge Handbook of African Linguistics.(Cambridge Handbooks in Language and Linguistics.) xxxi, 803 pp. Cambridge: Cambridge University Press, 2019. ISBN 978 1 108 41798 3. In: Bulletin of the School of Oriental and African Studies, 83(2), pp. 386-388. DOI: 10.1017/S0041977X20002335

♦ Saqwaré, Bu’ú, Paschal Bu’ú, Andrew Harvey, and Raheli Lawi. 2019. Koonkír Hhandoo. In: McCabe, Chris (ed.) Poems from the Edge of Extinction: an Anthology of Poetry in Endangered Languages. pp. 42-51. London: Chambers. Download

♦ Griscom, Richard, Andrew Harvey, and Anne Kruijt. 2020. Rift Valley Bibliography Version 1.3. DOI: 10.5281/zenodo.4300224  Pakua

Muhtasari
Kazi hii ni mkusanyiko wa machapisho kuhusu lugha za Eneo la Bonde la Ufa la Tanzania, ambapo lugha kutoka familia kubwa tatu za lugha za Kiafrika hupakana: Kinilo-Sahara, Kiniger-Kongo, na Kiafro-Asiatik, pamoja na Kisandawe (inayeweza kuwa na mahusiano na kundi la ‘Khoisan’, na Hadza, ‘lugha kisiwa’ ambaye haina mahusiano ya kijenetiki na lugha zingine.

♦ Harvey, Andrew. 2019. Harvey, Andrew. 2019. Gorwaa (Tanzania) – Language Contexts. In: Peter K Austin (ed.) Langauge Documentation and Description 16: 127-168. London, EL Publishing. PID: http://www.elpublishing.org/PID/171        Pakua

Muhtasari
Kazi hii ni jaribu la mwanaisimu kueleza lugha ya Kigorowa kwenye mazingira yake iliyeongelewa. Kwa kiasi kubwa, Kigorowa kinazungumzwa na watu takriban 133,000 wilayani Babati. Sio adimu kwamba wazungumzaji wa Kigorowa waweza kuongea Kiiraqw, Chasi, Kirangi, na moja au zaidi ya lahaja za Kidatooga, lakini karibu watu wote wanaoongea Kigorowa huongea Kiswahili pia. Tena, lugha ya Kiswahili inaendelea kuingia mahali pa Kigorowa kama lugha mkuu mjini, pamoja na vijijini. Kwa mfano, huko Babati mjini, watoto hawaongei lugha ya Kigorowa tena. Na hata kama mpisho wa Kigorowa kutoka wazazi kwa watoto unaendelea kijijini, bado Kigorowa kinapotea mawanda ya matumizi kwa Kiswahili. Wakati wazee wanaendelea kuona thamani ya kuongea Kigorowa, vijana wengi hawakithamini Kigorowa kama lugha ya ajira au nafasi ya kujiendeleza, mpaka huona aibu kukiongea Kigorowa kati ya watu wasiye wa jamii. Hatari ya Kigorowa kupotezwa inazidishwa kwa kuwa hakiandikwi kwa kawaida, na hifadhi yake pekee ni kongoo ya sauti na video ambaye mwandishi huyu ameunda yenyewe. Pia, kazi hii inasimulia kuhusu sura kadhaa za utamaduni wa Wagorowa, hasa zile zinazohusika na hali ya lugha. Sura hizi zinahusu: rasilimali na imani, uchumi, elimu, utaratibu wa uongozi na jamii, pamoja na udugu na ndoa. Kuonyesha upana wa lugha hii, namna mbalimbali ya kutumia Kigorowa zinaangaliwa kwenye kila kifungu. Kama mgeni, mawazo yangu yametegemea na uangalizi wangu pamoja na data zilizokusanywa kwa ajili ya utafiti wangu wa isimu. Kwa hiyo, somo hili ingeboreshwa tele kama, siku moja, mwanaisimu Mgorowa akisahihisha kazi yangu na ujuzi kutoka mazoezi ya maisha yake.

♦ Harvey, Andrew. 2018. Pakani: A Gorwaa story. In: The SOAS Journal of Postgraduate Research 11: Decolonisation in Praxis. pp. 153-184. Stable URL: http://eprints.soas.ac.uk/26318/        Pakua

Muhtasari
Muhtasari huu uko kwenye njia ya kutafsiriwa. Utakuwa tayari baadaye kidogo.

♦ Harvey, Andrew. 2018. The Gorwaa noun: Toward a description of the Gorwaa language. Doctoral dissertation, SOAS, University of London. DOI: 10.5281/zenodo.2527527        Pakua

Muhtasari
Muhtasari huu uko kwenye njia ya kutafsiriwa. Utakuwa tayari baadaye kidogo.

♦ Harvey, Andrew. 2018. Word-markers: toward a morphosyntactic description of the Gorwaa noun. SOAS Working Papers in Linguistics Vol. 19 pp.49-89. Stable URI: http://eprints.soas.ac.uk/id/eprint/26253       Pakua

Muhtasari
Muhtasari huu uko kwenye njia ya kutafsiriwa. Utakuwa tayari baadaye kidogo.

Harvey, Andrew. 2018. Maarten Mous: Alagwa – a South Cushitic language of Tanzania: Grammar, Texts and Lexicon. Journal of African Languages and Linguistics, 39(1), pp. 115-120. DOI: https://doi.org/10.1515/jall-2018-0007

♦ Harvey, Andrew, and Abel Yamwaka Mreta. 2016. Swahili Loanwords in Gorwaa and Iraqw: Phonological and Morphological Observations. In the Jarida la Kiswahili la TATAKI no.79. pp. 156-177. 2016. DOI: 10.5281/zenodo.2527517     Pakua

Muhtasari
Maneno ya Kiswahili yanapokopwa kwenda Kigorowa na Kiiraqw, kwa kawaida hutoholewa kufuatana na mtiririko wa miundo inayoweza kubainika. Kazi hii inaeleza namna maneno ya mikopo ya Kiswahili inavyoingizwa kifonetiki na kimofolojia kwenye lugha hizi mbili. Kifonetiki, fonimu ambazo hazipo kwenye Kigorowa na Kiiraqw hubadilishwa na sauti zinazofanana na sauti ya Kiswahili kwa sifa. Kama sauti inayofanana haipo kwenye Kigorowa na Kiiraqw, sauti ya Kiswahili huasiliwa. Kutohoa maneno ambayo huanza na konsonanti ya silabi ya nasal (syllabic nasal), aidha irabu huingizwa kutenganisha konsonanti zinazofuatana, au nazali ya mwanzo hufutwa. Mara nyingi, irabu hurefushwa kweye silabi yenye mkazo (ambayo, kwenye Kigorowa na Kiiraqw ni ya pili kutoka mwisho). Maneneo ya Kiswahili yasiyovunja kanuni za kifonolojia huongezwa kwenye Kigorowa na Kiiraqw bila mabadiliko. Kuhusu mofolojia, vitenzi vya mikopo hupewa kiambishi tamati nyambulishi (verbal derivational suffix) kuyatambua maneno haya kama vitenzi. Mfumo ya jinsi ya Kiswahili ni tofauti sana na ile ya Kigorowa na Kiiraqw, hivyo, ni lazima kila nomino mkopo kupewa jinsi. Kwa kawaida (lakini sio kila mara) hii hufanyika kufuatana umbo la kifonetiki la nomino. Nomino zinazoishia na irabu za umbo la duara hupewa jinsi ya kiume, na nomino zinazoishia na irabu za mbele hupewa jinsi ya kike. Kutengeneza uwingi kutoka maneno ambayo msingi yake ni umoja, au kutengeneza umoja kutoka maneno ambaye msingi yake ni uwingi ni vigumu zaidi kuelewa kwa sababu ya kanuni kadhaa zinazozalisha sana ambazo huyapa kiambishi tamati ya namba. Hii husababisha maumbo mengi ya ughairi.

♦ Harvey, Andrew. 2014. Epenthetic vowels in Swahili loanwords. In The Journal of Linguistics and Language Education, vol.8 no.2. pp 17-45 University of Dar es Salaam. DOI: 10.5281/zenodo.2527487     Pakua
ILANI: Kwenye chapisho la UDSM, kwa sababu ya kosa la uchapishaji sehemu za makala hazisomikani.  Toleo hili inasomekana kama ilivyokusudiwa.

Muhtasari
Wakati wa utohoaji wa maneno ya mikopo kwenda Kiswahili, irabu zinaweza kuingizwa. Matokeo yake ni maneno ambaye ni tofauti na yale ya lugha kopeshi (donor language). Kazi hii 1) inabainisha irabu zinazoingizwa, na 2) inafafanua mfumo ya udhihirishaji wa kifonetiki ya irabu hizi. Kama jina la makala inavyoeleza, irabu hizi ni za uchopekaji (epenthetic), sio za usazo (excrescent). Kwa kawaida, maneno yanapokopwa katika Kiswahili kwa njia ya uchopekaji, sifa (features) haziwezi kuvuka kutoka upande mmoja wa silabi yenye mkazo kwenda upande mwingine (ambayo kwa Kiswahili ni silabi ya pili kutoka mwisho). Kwa sababu hiyo, irabu za uchopekaji za mwisho ya neno hulazimishwa kuchukua sifa kutoka konsonanti ya karibu. Konsonanti zinazosambaza sifa za korona zinasababisha irabu ya uchopekaji ya korona [i], konsonanti zinazosambaza sifa la midomo zinasababisha irabu ya uchopekaji ya midomo [u], na konsonanti zinazosambaza sifa la koromeo zinasababisha irabu ya uchopekaji ya koromeo [a]. Konsonanti ya nyuma (dorsal) husambaza sifa lolote, na sifa za [korona] inaingizwa kama sauti ya msingi. Kwenye mazingira kabla ya mkazo, sifa za konsonanti pamoja na za irabu zinapatikana kwa ajili ya usambazaji wa sifa (Feature Spreading). Sifa za irabu yanasambazwa kwa urahisi zaidi kuliko sifa za konsonanti. Kwa hiyo, kwenye mazingira haya, usambazaji wa sifa za irabu kwenda irabu ya uchopekaji hutokea zaidi. Kuna maneno kadhaa ambapo inaonekana kwamba irabu za lugha kopeshi zinachukuliwa kama irabu ya uchopekaji. Baadhi ya maneno mbadala hayafuati kanuni inaokataza usambaaji wa sifa kutoka upande mmoja wa irabu yenye mkazo kwenda upande mwingine.