Kihadza (kinachojulikana pia kama Tindiga au Kangeju) ni lugha kisiwa (yaani: language isolate). Lugha hii huongelewa na watu takriban 1,000 kwenye Bonde la Ufa la Tanzania. Nilianza kusoma Kihadza mwaka 2019. Kinachofuata ni utangulizi wa lugha hii.
Gudo Mahiya anahadithia kuhusu nguruwe. [Kutoka Griscom and Harvey (forthcoming)]
Wahadza wameishi kwenye eneo linalozunguka Ziwa Eyasi kwa muda mrefu sana – mrefu zaidi kuliko vikundi vingine vyote vya eneo hili. Lakini sehemu wanapoishi imekuwa dogo sana kwa sababu ya kufika cha vikundi vingine. Leo hii, kwenye miji na vijiji vikubwa vya Uhadza (kama Mang’ola na Matala) kuna Wadatooga, Wairaqw, na watu wanaoongea lugha za Kibantu. Pia, uchungaji hukaribisha Wahadza na Wadatooga. Kwa upande wa magharibi, Wahadza wanapakana na Waihanzu.
Eneo la Ziwa Eyasi: Kihadza kinaongelewa hasa kwenye makambi karibu ya kijiji cha Mang’ola, kusini kwenye Sipunga kwa Bonde la Yaeda, kusini-magharibi kwa Tlhiika kwenye Milima ya Kidero, na kwenye upande wa kaskazini-magharibi wa Ziwa Eyasi kwa Dunduhina. Picha kutoka Google Maps.
Watafiti hawajahesabu idadi ya watu wanaoongea Kihadza, lakini masomo ya wanaanthropolijia yanaonyesha kwamba watu takriban 1,000 wanazungumza lugha hii. Hii nii idadi ya wazungumzaji wa Kihadza kubwa sana, lakini kwa sababu ya vitisho kwa ardhi yao na mtindo wao wa maisha, Kihadza bado ni lugha inayehatarishwa. Mipango ya kuwashawishi Wahadza kubadilisha maisha yao ya kuhamahama kwa maisha ya kilimo; upotevu wa ardhi kwa kilimo, ufugaji, na mbuga za wanyama; na mfumo wa utalii unaoweka bei kwenye maisha na utamaduni wa Wahadza huathiri afya ya watu, sehemu za asili zao, pamoja na nguvu ya lugha.
Picha ya Mariamu Anyawire, Machi 13, 2016. [Picha 20160313c (Griscom and Harvey, forthcoming)]
Wahadza ni maarufu kwa mtindo wao wa maisha wa uwindaji na ukusanyaji: hukusanya matunda na huchimba mizizi, na huwinda wanyama wadogo na wakubwa. Pia Wahadza hukaa kwenye makambi madogo yasiozidi watu thelathini, yanayohama mara kadhaa kwenye mwaka mmoja.
Kwa sababu ya konsonanti zake za vidoko, pamoja na mtindo wa maisha wa kuwinda na kukusanya, watu walifikiri kwamba Kihadza kilikuwa kwenye kundi la lugha za Kikhoisan. Sasa wazo hii haiaminiki tena, na inaonekana kwamba Kihadza ni lugha kisiwa (yaani: language isolate). Kifonetiki, Kihadza kina mfumo wa vokali 7, konsonanti za chemba mapafu (yaani: pulmonic consonants) 45, na konsonanti zisizo za chemba mapafu (yaani: non-pulmonic consonants) za ‘vidoko’ 9. Pia kuna tofauti kati ya toni juu na toni chini (yaani: high tone and low tone). Kisintaksi, mpangilio wa maneno wa Kihadza una umbo huru (yaani: non-configurational). Pia, inasemekana kwamba Kihadza, pamoja na rejista yake ya kuongea, kina rejista mbili za muluzi (yaani: whistled registers): mmoja inachotumika wakati wa kuwinda, na mmoja inachotumika wakati wa usiku tu. Ugunduzi zaidi utakuja na uchambuzi wingine.