Makala Zingine

Mkusanyiko wa data:

Harvey, Andrew. 2022. Gorwaa DoReCo dataset. In Seifart, Frank, Ludger Paschen and Matthew Stave (eds.). Language Documentation Reference Corpus (DoReCo) 1.2. Berlin & Lyon: Leibniz-Zentrum Allgemeine Sprachwissenschaft & laboratoire Dynamique Du Langage (UMR5596, CNRS & Université Lyon 2) DOI: 10.34847/nkl.a4b4ijj2

Muhtasari
Mkusanyiko wa data wa DoReCo wa Kigorowa ulikusanywa na Andrew Harvey kati ya miaka 2013 na 2016 na ulichambuliwa zaidi na timu ya DoReCo (hasa Laura Schleicher, Aleksandr Schramberger, Ludger Paschen, na Matthew stave) kati ya miaka 2019 na 2022. Faili ambazo DoReCo hutengeneza ni sehemu ndogo ya mkusanyiko mkubwa zaidi wa data za Kigorowa za Andrew Harvey zilizohifadhiwa kwenye ELAR (http://hdl.handle.net/2196/00-0000-0000-000F-79D0-1)

Makala:

Harvey, Andrew. 2022. An Ethnography for Fad Diets. In: Africa is a Country. Published 29.03.2022 Kiungo: https://africasacountry.com/2022/03/an-ethnography-for-fad-diets

Muhtasari
Watalii wawili walinunua safari ya kuwaona Wahadzabe, na walichoona kimewafurahisha mpaka wakatengeneza podcast. Kipi kinachoweza kuharibika?

Mkusanyiko wa Data:

Malleyeck, Herman, and Andrew Harvey. 2021. A dataset of personal names in Gisamjanga Datooga. Kiungo: 10.5281/zenodo.7770254

Muhtasari
Mkusanyiko huu wa data huchukua nukuu na rekodi zilizotengenezwa mji wa Haydom, mkoa wa Manyara, nchi ya Tanzania kwa Herman Malleyeck (mzungumzaji wa lugha ya Kidatooga aina ya Gisamjanga) na Andrew Harvey (mwanaisimu, lakini sio mtaalam wa Gisamjanga wala aina yoyote nyingine ya Kidatooga). Data zilikusanywa kwenye mwezi wa nne mwaka 2021, kutokana na orodha lililoandikwa na Herman Malleyeck.

Pamoja na data kwenye daftari ni: 1) jina kwenye Kidatooga cha Gisamjanga, 2) nadharia ya chanzo chake, 3) matokeo yanayoweza kusababisha mtoto kupewa jina hilo, na 4) mbadala kwa jina hii kwenye rejista ya ging’aweakshooda. Data zote na nadharia zote zilitengenezwa na Malleyeck.

Rekodi ni ya Herman Malleyeck akiyatamka majina kwenye daftari.

Makala:

Harvey, Andrew. 2021. Gikuyu in Catalonia. In: Africa is a Country. Published 05.03.2021 Kiungo: https://africasacountry.com/2021/05/gikuyu-in-catalonia

Muhtasari
Upotevu wa lugha za Kiafrika, uhusiano wao na utambulishaji, na kazi yao kuupinga ukoloni kwenye siku zitakazokuja.

Ripoti:

Harvey, Andrew and Richard Griscom. 2020. Haydom language documentation training workshop – January 2020: a report. DOI: 10.5281/zenodo.3971733     Pakua

Tambua kwamba: Ripoti hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kikao cha mafundisho ya kurekodi lugha mjini Haydom ilikuwa kikao cha siku tano kwa ajili ya kufundisha wazungumzaji wa lugha za Kitanzania Kinyisanzu na Kihadza kutafuta lugha zao kwenye majamii yao. Ripoti hii hueleza siku za kikao, pamoja na hutoa mawazo na hushiriki shauri kwa ajili ya wanaotaka kufanya kikao kama hii, hasa kwenye mazingira yenye uhaba wa vitu kama Intaneti na umeme.

Nakala ya Gazeti:
Harvey, Andrew. 2019. “Lessons from the field.” The ACU Review. 06/12/2019 Kiungo: https://www.acu.ac.uk/the-acu-review/lessons-from-the-field/

Wimbo wa Kigorowa kwenye Tangazo la Redio:

Rasper, Anke. 2019. “Protecting the world’s languages.” In: Rasper, Anke, and Lovely Wright “World in Progress: Keeping endangered languages alive”. Deutsche Welle 13/11/2019.

Kiungo: https://www.dw.com/en/world-in-progress-keeping-endangered-languages-alive/av-51229987

Sikiliza

Makala ya Blogu:
Harvey, Andrew, and Richard Griscom. 2019. “The Rift Valley Research Network: an introduction.” ELAR Blog. 20/06/2019 Kiungo: https://blogs.soas.ac.uk/elar/2019/06/20/the-rift-valley-research-network-an-introduction/

Podcast:
Tsutsui Billins, Martha, and Andrew Harvey. 2019. “Community collaboration for language documentation in the Tanzanian Rift Valley with Andrew Harvey.” Field Notes podcast. 11/06/2019 Kiungo: https://fieldnotespod.com/2019/06/11/ep-7-community-collaboration-for-language-documentation-in-the-tanzanian-rift-valley-with-andrew-harvey/

Makala ya Blogu:
Griscom, Richard, and Andrew Harvey. 2019. “Tanzanian community event on language documentation and endangerment.” ELAR Blog. 29/04/2019 Kiungo: https://blogs.soas.ac.uk/elar/2019/04/29/tanzanian-community-event-on-language-documentation-and-endangerment/

Makala ya Blogu:
Harvey, Andrew. 2019. “The world is flat, and all the best universities are at the top edge.’ The PIE Blog. 14/03/2019 Kiungo: https://blog.thepienews.com/2019/03/the-world-is-flat-and-all-the-best-universities-are-at-the-top-edge/

Ripoti:
Griscom, Richard, Andrew Harvey, and R. Lindfield. 2018. Report of Language Endangerment Workshop: Babati – July 2018 / Ripoti ya Kongamano la Lugha: Babati – Julai 2018. DOI: 10.5281/zenodo.2529349     Pakua(Kiingereza)     Pakua(Kiswahili)

Tambua kwamba: Ripoti hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mwezi wa Julai tarehe 16 na 17, 2018, wawakilishi kutoka makundi ya makabila manne kutoka katikati ya Tanzania walikutana Babati kujadili mabadiliko wanayokutana nayo siku hizi katika jamii zao na madhara yake katika lugha yao na utamaduni, vile vile na fursa za kupambana na mabadiliko yaliyo hasi. Makundi yaliyowakilishwa ni Waasimjeeg Datoga, Wagorwaa, Wahadzabe, na Wanyihanzu. Wagorwaa na Wanyihanzu walialikwa na Andrew Harvey, mtafiti aliyekuwa akifanya kazi ya kuhifadhi kumbukumbu ya lugha hizi. Waasimjeeg Datooga na Wahadzabe walialikwa na Richard Griscom, mtaalamu anayefanya kazi kaskazini mwa Tanzania na vikundi hivi viwili, kimsingi akitumia muda wake kuhifadhi kumbukumbu za Waasimjeeg Datooga. Makundi maawili yaani Wagorwaa na Waasimjeeg Datooga wana uzoefu kufanya utafiti wao wenyewe na Wanyihanzu na Wahadzabe wanajiandaa ambapo wataanza kufanya utafiti wao wenyewe. Malengo ya msingi ya kongamano ni kushirikishana uzoefu wa mabadiliko ya utamaduni, kuanzisha mtandao kati ya jamii tofauti zinazojihusisha katika utafiti wa lugha, kubadilishana maarifa na mafunzo kutoka miradi tofauti, na kujadili chaguzi mbalimbali kwa ajili ya uhusishaji unaowezekana na uhifadhi.

Makala ya Blogu:
Harvey, Andrew. 2016. “A day in the field – Andrew Harvey.’ ELAR Blog. 22/12/2016 Kiungo: blogs.soas.ac.uk/elar/2016/12/22/a-day-in-the-field-andrew-harvey

Ripoti:
Harvey, Andrew, Hezekiah Kodi, Josiah Sumaye, Raheli Lawi, Andrea Tsino, Paschal Bu’ú, Stephano Edward, and Festo Massani. 2016. Gorwaa Language Project: Action Plan I (2017-2022); Babati – August 2016 / Mradi wa Lugha ya Kigorowa: Mpango Kazi I (2017-2022); Babati – Agosti 2016 DOI: 10.5281/zenodo.2535899  Pakua(Kiingereza)  Pakua(Kiswahili)

Tambua kwamba: Ripoti hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mpango kazi ufuatao umekuja kama matokeo ya miaka mitano ya mahusiano ya karibu sana baina ya wajumbe wa Kamati ya Jamii ya Lugha ya Gorwaa (Josiah Sumaye, Hezekiah Kodi, Raheli Lawi, Andrea Tsino, Paschal Buu, Stephano Edward na Festo Massani, na Mtaalamu mtafiti wa kigeni wa Lugha Andrew Harvey). Mpango huu umekusudiwa kutumika kama wajibu kuakisi hali halisi ya upotevu wa lugha ya Gorowaa, pia kama njia kuelekea ufufuaji wa lugha na uboreshaji wake katika jamii.